Robo fainali klabu bingwa kupangwa leo - LEKULE

Breaking

20 Mar 2015

Robo fainali klabu bingwa kupangwa leo

Droo ya kupanga Mechi za robo fainali za uefa champion ligi itafanyika leo Jijini Nyon Uswisi, kuanzia Saa 8 Mchana.
Jumla ya vilabu nane kutoka Nchi 5 za Ulaya zipo kwenye Droo hiyo ambayo tofauti na Raundi zilizopita, safari hii ni huru na hivyo Klabu za Nchi moja hazibaguliwi na zinaweza kukutanishwa.
Hii itakua ni mara ya kwanza kwa miaka 22 iliyopita kukosekana kwa timu za England.
Mechi za Robo Fainali zitachezwa hapo Aprili 14 na 15 na Marudiano ni Aprili 21 na 22.
Droo ya Nusu Fainali itafanyika Aprili 24 na Mechi zake kuchezwa Mei 5 na 6 na Marudiano ni Mei 12 na 13.
Fainali ya michuano hii itachezwa Juni 6 katika dimba la Olympiastadion, Jijini Berlin, Ujerumani.

No comments: