Real Madrid ilishindwa kuchukua fursa ya uongozi wake katika ligi ya La Liga nchini Uhispania baada ya kunyukwa 1-0 na kilabu ya Athletic Bilbao katika uwanja wa San Mames.
Mshambuliaji wa kilabu ya Athletic Aritz Aduriz mwenye umri wa miaka 30 aliiweka kilabu ya nyumbani kifua mbele kwa kufunga kichwa kizuri baadsa ya kupata krosi safi kutoka kwa Mikel Ricos.
Real Madrid ilitawala ngoma hiyo baada ya kipindi cha pili ambapo mkwaju wa Gareth Bale uligonga mwamba.
Lakini Athletic Bilbao ilikaza kamba na kupata ushindi huo ambao sasa unaiweka kilabu ya Madrid juu na pointi 2 dhidi ya Barcelona.
Hii Inamaanisha kuwa Barcelona itapanda na kuchukua uongozi wa ligi hiyo iwapo itashinda mechi yake dhidi ya Rayo Volcano katika uwanja wa Nou Camp siku ya jumapili.
No comments:
Post a Comment