Pigo Jingine Kwa Chama Kipya Cha ACT-Tanzania: Baraza la Kilimo Lapinga ACT Kutumika Kama Jina la Chama - LEKULE

Breaking

27 Mar 2015

Pigo Jingine Kwa Chama Kipya Cha ACT-Tanzania: Baraza la Kilimo Lapinga ACT Kutumika Kama Jina la Chama

Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) limekitaka chama cha siasa cha ACT – Tanzania kutotumia jina hilo kwa kuwa tayari baraza hilo limekwsha sajili jina la ACT kama kifupi cha jina la Baraza hilo.

Akizungumza leo na  mwandishi wetu, Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt Sinare Yusuf Sinare amesema kuwa jina ACT linatambulika kama kifupi cha Agricultural Council of Tanzania na kwa mujibu wa taratibu za hati miliki, jina hilo (ACT) halitakiwi kutumika na watu wengine hata kama litaambatanishwa na maneno mengine.

“Hata kama wakiongeza maneno, bado kuna ACT, hiyo ni nembo yetu, tumekwisha andika barua kwenda kwa msajili wa vyama vya siasa, pia tumeandika barua kwenda katika chama hicho lakini bado hatujapata majibu, nimekwisha ongea na Zitto Kabwe kuhusu hilo na kumweleza kuwa wanatakiwa kurekebisha kabla hatujaenda hatua za juu zaidi(Mahakamani) ambazo ni ghali.” Amesema Dkt Sinare

No comments: