OYA MWANA, NDIMU CHANGA HAINA MAJI! - LEKULE

Breaking

20 Mar 2015

OYA MWANA, NDIMU CHANGA HAINA MAJI!


Mambo vipi wanangu wenyewe? Mzuksi? Kitaa hiyo kwa ndichi hapo kati inakuwa nini? Kipande hii haiwi kitu aisee. Hapa vumbi tu kama vipi welikamu kwa jamvini rede kukisanua. Kwani kuna tatizo? Hakuna tatizo!

Huku na huku kaka mkubwa nipo kitaa nimechili na wana. Si unanyaka zile za kula tu wepesi na makiksi wa kitaa? Wapo njema hatare, unaweza ukaua dheni ikawa soo kwa kitaa. Hapo ndo stori moo inahapeni.

Kenny ni kaka la kaka la kitaa kitambo. Tumezoeana bati hatujawahi kupiga mastori diipu. Sasa bana lasti wikiendi akaona anipige stori na Mpeke kuhusu mchongo f’lani hivi fekelo wa kuhusu braza’ke na kama vipi nimpe masolusheni.

Oya selaa festi zima fegi kozi baba la baba nina aleji dheni si imekatazwa kupiga hayo mavitu kwenye kadamnasi mazee? Sasa inakuwaje tena? Bifoo mwana Kenny hajaanza kunipa mchapo nikaona nijifanye nipo faya kozi truu mi sipo inlavu na moshi wa aina yoyote haijalishi fegi au sigara kubwa.
Hapo ndo sasa mwana nikampa maiki akaanza kutambaa.

Ebana kwenye famili yetu tupo mtu bee kwa maana ya makidi wa kiume. Wazazi majembe!
Braza ninayemfuata amefunga kitu cha pingu za laifu tena kwa pati kubwa hatare. Pipo walipiga mpunga kitenesi usipime.

Ebana mereji yao imesavaivu miaka bee nawu bila vurugu mechi zilizozoeleka tudei. Unanyaka nawu deizi mereji hazidumu sijui kwa nini! Sasa bana mpango mzima wa mboyoyo mingi kati yao umeibuka juzikati kozi mama la mama wa selaa yupo kwenye taimu mbaya kinoma.

Shemu la mashemu amekuwa ni mtu wa kupiga mambo hadi anakuwa bwaksi yaani inaitwa weka mbali na makidi.Broo akiibuka homu anamkuta waifu yupo nyingi na hajitambui kabisa na amekuwa akiendeleza matingasi na mara zote nimekuwa nikimpiga chabo akimchenjia braza hadi panachimbika kinoma.

Aisee wamekuwa wakisuluishwa na maparenti deile bati ndo kama hivyo mawota yakishamwagika huwezi kuyachota ukajaza kwenye gunia na kama ndimu ni changa kamwe haiwezi kutoa au kuwa na maji. Kuna vitu imposibo tu hata ufanyeje.

Nikaona isiwe kitu, nikaamua kufanya mauchunguzi kujua nini sheeda hadi braza anazinguana na maza wa makidi wake?Katika marisechi yangu ndo nikasanuka kumbe shemu anachiti na bizinesimani mmoko femasi kishenzi kwa fasi ya kitaa.

Ili kujipa mauhakika nikaanza kumfuatilia waifu wa broo hadi nikamfuma laivu kunako hoteli akila maraha na msela.Mazee ishu nainyaka freshi bati inakuwa ngumu masela wanasema ngumu kumeza.

Nitaanzia wapi kumweleza braza ishu mbaya kaa hiyo? Huu si ni mtihani jamani? Kama ni wewe ungechukua stepu gani? Tafakari dheni chukua hatua! Nimemaliza.Ebana mmemsoma mwana? Tupia maushauri kwenye foni hapo juu dheni yatamfikia kachala wako.

No comments: