Niger na Chad zashambulia Boko Haram - LEKULE

Breaking

8 Mar 2015

Niger na Chad zashambulia Boko Haram


Wanajeshi wa Niger na Chad wamefanya mashambulio angani na ardhini kaskazini-mashariki mwa Nigeria dhidi ya wapiganaji Waislamu, Boko Haram.

Mkaazi wa Diffa nchini Niger, alisema kuwa aliwaona wanajeshi wakielekea mpakani asubuhi Jumapili na akasikia milio ya bunduki.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Niger kuingia ndani sana Nigeria, wakati kabla wakipigana na Boko Haram eneo la mpakani tu.

Ijumaa, Umoja wa Afrika uliidhinisha kuunda kikosi cha Afrika cha wanajeshi kama 8,000 kupambana na tishio linalozidi kutoka Boko Haram.

Serikali ya Nigeria imesema kuwa tangazo la wapiganaji wa Boko Haram la kuahidi utiifu kwa Islamic State, linaonesha kuwa wapiganaji hao wa Nigeria wamebanwa.

Msemaji wa serikali, Mike Omeri, aliiambia BBC kwamba Boko Haram imepata hasara kubwa na kupoteza nguvu zake, kwa sababu ya mashambulio ya majeshi ya Nigeria na ya nchi jirani.

Ahadi hiyo ya utiifu ilitolewa Jumamosi na kiongozi wa Boko Haram, Abubukar Shekau, kwenye ujumbe uliowekwa katika mtandao wa internet.

Bwana Omeri alisema tangazo hilo ni jaribio la Boko Haram kuomba msaada katika vita vyake na taifa la Nigeria.

No comments: