Netanyahu kuhutubia Congress leo - LEKULE

Breaking

3 Mar 2015

Netanyahu kuhutubia Congress leo


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amethibitisha kwamba atapinga mpango wa Nyuklia wa Iran pindi atakapohutubia bunge la congress hii leo.

Amesema katu hato unyamazia mradi ambao unahatarisha maisha ya waisrael.

Bwana Netanyahu ametoa kauli hiyo pindi alipokuwa akihutubia shirika linalounga mkono Israel lililopo mjini Washington

Wakati huo huo, Netanyahu amethibitisha kutokubaliana na Ikulu ya Marekani kuhusu jinsi gani ya kuizuia Iran isiendeleze mpango wake wa Nyuklia. Lakini amesema vyovyote itakavyokuwa, Israel haitakubali Iran kuendeleza mpango wake.

Kwa Upande wake Rais wa Marekani Barack Obama amesema kumekuwa na hali ya kutokukubaliana kati ya Marekani na Israel kuhusu njia bora ya kuifanya Iran isizalishe silaha za Nyuklia.

Lakini akizungumza na Shirika la Habari la Uingereza Reuters kabla ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kulihutubia Bunge la Congress, amesema hakufikiri kutofautiana huku kungeharibu mahusiano kati ya Washington na mshirika wake wa karibu katika eneo la Mashariki ya kati.

Obama ametaka kusimamishwa kwa mpango wa Nyuklia wa Iran kwa miaka 10, Israel inaamini kuwa kuwa makubaliano yanayofanya Iran kuendelea kuwa na viwanda vyenye kuzalisha Nyuklia ni hatari.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema Israel inahatarisha mchakato wa mazungumzo ikiwa itaamua kuchagua baadhi ya vipengele katika mazungumzo hayo.

No comments: