MWILI WA ABDUL BONGE WAHAMISHIWA MUHIMBILI KWA UCHUNGUZI - LEKULE

Breaking

30 Mar 2015

MWILI WA ABDUL BONGE WAHAMISHIWA MUHIMBILI KWA UCHUNGUZI


Mwili wa Abdu Bonge ukitolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwanyamala jijini Dar ili kuhamishiwa Muhimbili.

Ukiwa ndani ya gari kwa ajili ya kupelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Ndugu wakijiandaa na safari.

Safari ilivyoanza kuelekea Muhimbili

MWILI wa aliyekuwa mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdu Bonge, mapema leo asubuhi ulihamishwa kutoka katika Hospitali ya Mwananyamala na kupelekwa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Mtandao huu ulishuhudia jamaa wa marehemu huyo wakiuhamisha mwili huo wakisema ni lazima mwili huo ukafanyiwe uchunguzi wa kina kutokana na utata wa kifo chake.

Mdogo wa marehemu aitwae Idd Taletale alisema endapo uchunguzi huo utamalizika leo utasafirishwa leo kuelekea Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.

No comments: