MVUA inayoendelea kunyesha jijini Dar, tayari imeanza kusababisha kero kwa wakazi wa jiji hilo kufuatia mitaro ya maji machafu kufurika na kuwafanya watu washindwe kutumia vizuri barabara.
Miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa na mvua hiyo ni pamoja na Sinza, Afrika-Sana na Bamaga-Mwenge ambapo mwanahabari wetu alishuhudia wananchi wakipata usumbufu wa kuvuka barabara zilizojaa maji hali ambayo imesababisha washindwe kufika katika shughuli zao kwa wakati.
No comments:
Post a Comment