Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India - LEKULE

Breaking

27 Mar 2015

Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India


Amini usiamini mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameweka rekodi ya taifa ya ulengaji shabaha kwa mishale nchini India.
Kulingana na vitabu vya kumbukumbu ya rekodi za taifa, Dolly Shivani Cherukuri kutoka Vijaywada katika jimbo la Andhra Pradesh
aliweka rekodi ya kuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi kusajili alama 200 katika mashindano yaliyoandaliwa jumanne iliyopita.
Kulingana na jarida la Press Trust la India ,mtoto huyo alifuma mishale 36 kutoka umbali wa mita 5 na kisha umbali wa mita 7 na kujizolea alama 388.
Tukio hilo lilishuhudiwa na wachezaji wakongwe na maafisa kutoka idara ya kumbukumbu za michezo.
''kwa hakika tunajivunia matokeo haya ''alisema afisa wa shirikisho la mishale la India bwana Gunjan Abrol.
Dolly ambaye alizaliwa baada ya kupandikizwa kwa mbegu ya babake kufuatia kifo cha kakake katika ajali ya barabarani.

Kakake alikuwa mrushaji mishale wa kimataifa Cherukuri Lenin.
Babake Cherukuri Satyanarayana ,anasema kuwa Dolly alifunzwa kufuma mishale, tangu alipozaliwa.
Babake ni mmiliki wa klabu kimoja kinachofunza kurusha mishale.
Aidha aliiambia shrika la habari la AFP kuwa kitambo alikuwa amemptengezea uta na mishale nyepesi ilikukuza talanta ya mtoto huyo.
Sasa babake anasema kuwa anapanga kumshirikisha mwanawe katika mashindano kwa nia ya kumsajili katika vitabu vya rekodi za dunia za Guinness.

No comments: