Bingwa wa mbio ndefu za kilomita 42 za Kilimanjaro Full Marathon, Fabiola Willium akimaliza mbio hizo katika mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi leo.
Mshindi wa mbio ndefu za Kilomita 42 za Kilimanjaro Full Marathon, David Ruto akimaliza mbio hizo katika mashindano yalika Moshi leo.
Washiriki wa mbio fupi za Kilomita 21 za Tigo Half Kili Marathon wakichuana wakati wa mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon 2015 zilizofanyika Moshi
MTANZANIA
FABIOLA
WILLIUM
ATWAA
DHAHABU
MBIO
ZA
KILIMANJARO
MARATHON
HII
LEO
Bingwa wa mbio ndefu za kilomita 42 za Kilimanjaro Full Marathon, Fabiola Willium akimaliza mbio hizo katika mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi leo.
Mshindi wa mbio ndefu za Kilomita 42 za Kilimanjaro Full Marathon, David Ruto akimaliza mbio hizo katika mashindano yalika Moshi leo.
Washiriki wa mbio fupi za Kilomita 21 za Tigo Half Kili Marathon wakichuana wakati wa mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon 2015 zilizofanyika Moshi
**************
Mwana dada wa Tanzania Fabiola William (32),ameibuka mshindi wa kilomita 42 (Full Marathon woman) katika mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika leo katika viunga vya mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Fabiola ametumia muda wa saa 2:49:51 na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 4 kutoka kwa wadhamini Kilimanjaro Lager na kuwaburuza wakenya Rosaline David, Joan Cherop, Dorice Todipus, Sarah Maiyo , Gladys Cheruiyo , Susan Koskei, Julitter Tanin, Esther Mutuku na Lilian Chelimo walioshika namba 2 hadi 10.
Full Marathon wanaume, David Ruto (Kenya), aliibukamshindi baada ya kutumia 2:15:50 na kuzawadiwa Sh milioni 4 huku nafasi ya pili hadi ya tano zikienda Kenya kwa wakimbiaji, Benard Kimayo, Alex Bartida, George Ngure na Douglas Chebii.
Mtanzania Pascal Mombo alijitokeza na kushika nafasi ya sita huku wakenya David Kilimo, Lawrence Rotich, Mathew Koskei wakichukuanafasi ya 7 hadi 9 na Mtanzania Siegried Ngolly kumaliza wa kumi.
Aidha katika mbio za Kilomita 21, nafasi ya kwanza hadi ya nne ilikwenda kwa Watanzania, Ismail Juma, Emmanuel Giniki, Theotil Joseph, Felix Alfonse huku nafasi tano hadi ya nane ikienda Kenya kupitia Festus Stalamestus, Vicent Kipruto, Fanuel Mkungo na Dickson Kimuthi, Mtanzania Elia Sidame alimaliza wa tisa na mkenya Martin Muhinde kumaliza wa kumi.
Upande wa wanawake Half Marathon Kilomita 21, wakim,biaji wa Kenya walifanya vyema kwa kuchukua tano bora ikiongozwa na Grace Kimanzi ,Yunice Echumba, Vicoty Cherkemai, Sherekith Nyawera, Jane Mwikal.
Nafasi ya sita hadi ya nane ilikwenda kwa watanzania Failuna Abdi, Mary Naali na Catherine Lange na tisa na kumi zikenda Kenya Yunice Mutie na Ludera Fida.
Akizungumza katika mbio hizo, mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, alisema aliwapongeza waandaaji wa tukio hilo la aina yake.
“Nawapongeza sana wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager, waandaaji na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja mmefanikisha mbio hizi kwa miaka 13 sasa,” alisema.
Pia aliwapongeza GAPCO kwa kudhamini mbio za walemavu pamoja na wadhamini wengine ikiwemo Grand Malt, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, Kibo Palace Hotel, UNFPA, Kilimanjaro Water, pamoja na wadhamini shirikishi wapya kabisa katika mbio hizi ambao ni NSSF na Tanzania Coffee Board.
No comments:
Post a Comment