Kocha wa Chelsea amewaonya wapinzani wake akisema kuwa bado anaari kubwa ya kutwaa vikombe zaidi.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amewatahadharisha wapinzani wake kuwa ataendelea kutafuta mataji zaidi wala hatalegeza kamba kamwe licha ya kutwaa tuzo la Capital One.
Katika kipute hicho vijana wa kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho waliandikisha bao la kwanza katika dakika ya 45 ya mchezo huo kupitia kwa nahodha wake John Terry.
Timu hizo zilikwenda mapumzikoni matokeo yakiwa hayo.
Katika kuthibisha kuwa siku ya kufa nyani miti yote huteleza, dakika ya 56 mlinzi wa Tottenham Kyle Walker aliwahakikishia vijana wa darajani ushindi wa kishindo baada ya kujifunga katika harakati za kuokoa hatari kutoka
langoni mwake.
Kombe hili ni la kwanza kwa kocha Mourinho tangu ajiunge kwa mara nyingine na klabu hiyo mwaka 2013 akitokea nchini Hispania alikokuwa akiifundisha miamba ya soka nchini humo Real Madrid.
Aidha ni tuzo la 21 la meneja huyo machachari.
" nahisi vile kama mtoto akishinda tuzo lake la kwanza ,"
''Ni vigumu kuishi pasi na kutwaa matuzo''
''nafikiri nahitaji kutumia tuzo hizi kwa chajio ,ushanielewa ?
Kocha huyo alilisikika akisema.
Mourinho, ambaye alikuwa mkufunzi Stamford Bridge kati ya 2004 na 2007sasa ameingoza klabu hiyo kutwaa mataji 7.
The Blues wanawaongoza Manchester City kwa zaidi ya alama 5 kileleni mwa jedwali la ligi.
Kwa upande wao City waliambulia kichapo cha 2-1 mikononi mwa Liverpool jumapili.
''ndio mwanzo mkoko umealika maua'' alisema nahodha wa Chelsea Terry.
Nimeshinda vikombe vingi sana nitavitumia kwa chakula
Mourinho
Mataji aliyotwaa Mourinho
Ligi ya Premia
2004-05, 2005-06
FA
2006-07
League Cup
2004-05, 2006-07, 2014-15
FA Community Shield
2005
No comments:
Post a Comment