Migodi kumi na tano yateketea kwa moto mererani wilayani Simanjiro. - LEKULE

Breaking

9 Mar 2015

Migodi kumi na tano yateketea kwa moto mererani wilayani Simanjiro.


Zaidi ya migodi kumi na tano ya wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite kitaru B kwenye machimbo ya mererani wilayani Simanjiro imeteketea kwa moto unaodaiwa kutokana na itirafu ya umeme na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni nne na watu elfu mbili kukosa ajaira.
ITV ilifika katika migodi hiyo na kushuhudia majengo mitambo ya vifaa vingine vikiwa vimeteketea kwa moto na wasimamizi wa migodi hiyo wakaeleza namna moto huo ulivyo anza huku wakidai kuwa ulilipuka wakati wafanyakazi wa Tanesco walipokuwa wanafanya matengenezo ambao baada ya moto kuwaka wamedaiwa kukimbia katika eneo ilo.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya usuhuishi na usalama wa migodi katika kitalu B Neene Lymo amesema hasara waliyoipata ya zaidi ya shilingi bilioni nne ni kubwa hivyo wameitaka serikali iwasaidie kwa kuwalipa fidia kwakuwa chanzo ni shirika la umma huku wamiliki wa migodi hiyo wakidai kuna hujuma katika tukio ilo.

Mkaguzi wa migodi na baruti kutoka wizara ya nishati na madini Henri Mditi amesema wataalam wa wizara wamefika na kuona eneo lililo athirika lakini taarifa zaidi zitatolewa na kamishina wa madini kanda ya kaskazini baada ya ukaguzi kukamilika.

ITV bado inafanya juhudi za kuutafuta uongozi wa shirika la Tanesco mkoa wa Manyara ili kupata ufafanuzi wa tukio ilo.

No comments: