Mcheza Filamu wa Hollywood,apata ajali - LEKULE

Breaking

6 Mar 2015

Mcheza Filamu wa Hollywood,apata ajali


Mcheza filamu wa Hollywood,Harrison Ford, anapatiwa matibabu katika Hospitali moja mjini Los Angels baada ya ndege yake kuukuu kuanguka katika uwanja wa Gofu.

Mcheza filamu huyo mwenye umri wa miaka 72 alikuwa akiendesha ndege hiyo mwenyewe.

Ndege hiyo ndogo ilinasa kwenye mti wakati ilipokuwa ikitua kwa dharula.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema Harrison Ford alikuwa amejeruhiwa, akionekana kuwa na damu iliyotapakaa usoni.

Matabibu wamesema Ford anaendelea vizuri na kuwa hali yake itatengemaa kabisa.

No comments: