Matumaini ya Serikali juu ya ndege ya Malaysia Airlines MH370 - LEKULE

Breaking

8 Mar 2015

Matumaini ya Serikali juu ya ndege ya Malaysia Airlines MH370



Kutimia mwaka mmoja tangu lilipotokea tukio la kusikitisha la kupotea kwa ndege ya Malaysia Airlines MH370 ambayo ilipotea tarehe 8 March 2014 ikiwa imebeba abiria 239 kutoka Malaysia kwenda China.

Mweza January 2015 Serikali ya Malaysia ilitangaza rasmi kwamba jitihada za kuitafuta hazikuwa na dalili wala matumaini yoyote kuipata, lakini katika mahojiano aliyoyafanya na Shirika la Utangazaji la BBC, Liow Tiong Lai Waziri wa Uchukuzi wa Malaysia amesema bado vikosi vya utafutaji vinaendelea na kazi ya kuitafuta ndege hiyo ambapo kazi hiyo wanashirikiana na Serikali ya Australia.

Waziri anaamini mpaka kufikia mwezi May mwaka huu kazi ya kuitafuta itakuwa imekamilika na watakuwa wameipata ndege hiyo; “We are confident we can complete the search hopefully by May this year, and we hope we can get the plane“– Liow Tiong Lai.

No comments: