Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje
wa Marekani, John Kerry, amesema kuwa Marekani hatimae itabidi
kuzungumza na rais wa Syria, Bashar al-Assad, ili kumaliza vita vya
wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Katika mahojiano yaliyooneshwa
kwenye televisheni, Bwana Kerry alisema mazungumzo ya awali ya kumaliza
vita hayakufanikiwa kwa sababu rais wa Syria hakuwa tayari kuzungumza.Vita vya Syria sasa vinaingia mwaka wa tano.
Hapo awali Marekani ikisisitiza kuwa kuwa Rais Assad lazima ajiuzulu, kama sehemu ya suluhu ya kisiasa.
Maneno ya Bwana Kerry yanafuata matamshi ya mkurugenzi wa idara ya ujasusi, CIA.
Juma lilopita John Brennan alisema Marekani haitaki Rais Assad ashindwe kwa sababu inaweza kuwasaidia wapiganaji wa Islamic State kupata nguvu zaidi.
Umoja wa Mataifa unakisia kuwa watu zaidi ya 200,000 wamekufa katika vita hivyo na karibu nusu ya wananchi wa Syria wamehama makwao.
No comments:
Post a Comment