Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuwa wazi kuanzia hatua ya kujiandikisha kupiga kura ili kuepuka malalamiko dhidi ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Mbunge huyo wa Bumbuli alisema hayo jana katika mdahalo ulioandaliwa na taasisi ya Rich Management kuhusu uongozi unaohitajika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
Makamba alisema mara nyingi kunakuwa na maswali mengi yasiyo na majibu katika hatua mbalimbali za uchaguzi, kitu ambacho alisema husababisha mgogoro na kutoelewana wakati wa kutangaza matokeo.
“Uchaguzi ni suala muhimu na la lazima, sasa mipango madhubuti inahitajika ili kuhakikisha hakuna nyufa zinazoweza kuuvuruga, ”alisema.
Pia aliwataka viongozi wanaowania nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao, wawe wazi na wakubali kuhojiwa badala ya kufanya mambo kwa kificho.
“Kama mtu ni msafi hana haja ya kujificha, ndiyo maana mimi nilitangaza wazi kuwa nataka kugombea urais, haina haja ya viongozi kukwepa mahojiano na wananchi,” alisema Mkamba.
Makamba pia aliwataka wananchi kutokubali kurubuniwa kuchagua viongozi walionunua kura zao kwa kutumia fedha badala ya kujitambulisha kwa utendaji.
Alisema wananchi wachague viongozi wasafi wenye sifa na walio tayari kuwa watumishi, wahudumu katika jamii, badala ya kuchagua viongozi watawala.
Maoni ya Makamba yaliungwa mkono na wakili kutoka kampuni ya Crax Law Partners, Hamza Jabi ambaye alisema midahalo kama hiyo ni mizuri, hasa ikiwa inafanywa na vijana wenye malengo ya kuwa viongozi ili kuwapa changamoto vijana wengine kujifunza na kutaka kujua mambo mengi zaidi.
“Naamini katika viongozi vijana, wanatoa njia kwa wengine na wanaongoza kulingana na dunia ya sasa badala ya kuongoza kwa uzamani, ”alisema Wakili Jabir.
Mfanyabiashara Matlida kwayu alisema midahalo kama hiyo huwajenga wanaofahamu na wasiofahamu kwa kusikia kinachotakiwa kufanywa huku wakijiongezea kujiamini na kujijenga kiakili kufanya maamuzi sahihi.
Naye Wakili Soba Sang’anya alisema kama ambavyo Makamba amezungumza wananchi ndiyo wana haki ya kufanya uamuzi sahihi kwa kuchagua viongozi bora na wasafi.

No comments:
Post a Comment