MACHINGA, WAUZA MAGAZETI WACHUKULIWA MALI ZAO JIJINI MWANZA - LEKULE

Breaking

22 Mar 2015

MACHINGA, WAUZA MAGAZETI WACHUKULIWA MALI ZAO JIJINI MWANZA

Polisi na askari wa Jiji la Mwanza wakiwa wamekusanya mali za machinga na kuzipakia kwenye gari.
Baadhi ya machinga waliokamatwa wakiwa kwenye gari la polisi.
Magari ya polisi yakiwa na mali za machinga.
Askari wa Jiji la Mwanza akipanda kwenye gari tayari kuondoka eneo hilo.
Askari wa Jiji la Mwanza wakitokomea na mali za machinga

WAUZA magazeti na wafanyabiashara wadogowadogo hapa jijini Mwanza maarufu kama Machinga jana wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na polisi pamoja na maaskari wa jiji hilo na kuanza kupakia bidhaa zao bila ya kutoa taarifa hali inayopelekea maendeleo ya wananchi hao kurudi nyuma kila kukicha.

Wakizungumza na vyombo vya habari wafanyabiashara hao wamesema kuwa “Sisi tumekuwa tukifanya biashara zetu hizi ndogondogo hapa kwa muda mrefu sasa na wengi wetu tumesomesha watoto wetu tukiwa hapa hapa sasa hawa viongozi wanaokuja na kubeba vitu vyetu wanataka tuishije? Walihoji wafanyabiashara hao.

Ikumbukwe kwamba wafanyabiashara wadogowadogo katika jiji hili wamekuwa hawaelewani na viongozi wa jiji hasa Mkurugenzi wa jiji hilo kwa madai kuwa anawanyanyasa kwani hapo ndipo wanapopata riziki zao za kila siku "Kwa kweli sisi tumechoka kwani kila siku tunahemea bidhaa ili tuone kama tunaweza kuishi lakini kumbe watu wengine wanapanga kuturudisha nyuma na hii inaonekana wazi kuwa serikali imetuchoka kwani endapo tutatoka hapa na kuanza kufanya matendo maovu serikali wataanza kuchonga wakati hali hiyo wanaisababisha wenyewe." waliongeza wafanyabiashara hao.

Aidha kumbakumba hiyo ya kukamata mali za wafanyabiashara hao imewakumba pia wauza magazeti, wauza matunda na mafundi viatu katika maeneo ya stendi ya ya magari yatokayo Igoma kwenda uwanja wa ndege, Mwanza Hotel mkabala na Gold Crest Hotel na Barabara ya kuelekea Hospitali ya Mwananchi karibu na zilizopokuwa ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) jijini hapa.

Katika hatua nyingine, mmoja wa wafanyabiashara aitwaye Joseph Mzuri amemuomba Mbunge wa Jimbo la Nyamagana kuhakikisha anapigana na hawa watu ambao hawataki wananchi wenye kipato cha chini wapate mafanikio.

No comments: