Liverpool yailaza Mancity - LEKULE

Breaking

1 Mar 2015

Liverpool yailaza Mancity



Phillipe Coutinho alifunga bao la ushindi na kuiwezesha Liverpool kuharibu matumaini ya Mancity kulitetea taji lake katika uwanja wa Anfield..

Bao la Jordan Henderson liliiweka mbele Liverpool kabla ya Edwin Dzeko kusawazisha.

Lakini Mchezaji wa Brazil Coutinho alipachika bao la kuvutia alipofunga kutoka nje ya eneo la hatari.

Matokeo hayo yanaiweka Mancity pointi 5 nyuma ya Chelsea huku wakiwa wamecheza mechi moja zaidi nayo Liverpool ikipanda hadi nafasi ya tano katika jedwali.

No comments: