KWA HILI LA KITAMBI KUMRIDHI OMODG,AZAM MMEBUGI - LEKULE

Breaking

14 Mar 2015

KWA HILI LA KITAMBI KUMRIDHI OMODG,AZAM MMEBUGI


Habari za leo Msomaji wetu , Labda nianze tu kwa kukumbusha msemo wa Mababu zetu “Mficha Ugonjwa, Kifo Humuumbua, na Mchagua nazi Huibukia Koroma” bila kupinga hivyo ndivyo ilivyo.
Toka mwaka 2007 klabu ya Azam FC, ilipofanikiwa kutinga katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Watanzania wengi hasa wenyenia ya dhati na Maendeleo ya Soka letu, Waliiamini Timu hiyo inayomirikiwa na Kampuni ya Bakhresa Group Company, Wakisema kuwa ndio mkombozi wa kabumbu la ardhi ya Kikwete, labda tu kutokana na miundombinu pamoja na mipango na mikakati ambayo Azam FC ilijiwekea ikiwemo kukuza na kuendeleza Soka la Tanzania sambamba na kufika mbali katika michuano ya Kimataifa.
Kwahili Azam Mmechemka.
Wakiwa na ndoto za kutaka kuwa na mafaniio Kisoka kama Timu za TP Mazembe ya DRC na nyingine za Barani Afrika, Wiki chache zilizo pita klabu hii ambayo ndio Matajili wa Ligi kuu ya Tanzania bara pengine hata ukanda wa Afrika Mashariki, Walichukua uamuzi mzito wa kumtimua kazi aliyekuwa kocha wao Mkuu RAIA wa Cameroon Joseph Omog, ikiwa ni siku mbili tu baada ya kutolewa katika michuano ya klabu Bingwa na Al Merreikh ya Sudani kwa jumla ya mabao 3-2.

Kwa upande wangu, Kufukuzwa Omog katika kikosi hicho sikushituka sana, kwani najua Makocha wanaajiliwa na kufukuzwa pindi wanaposhindwa kufikia malengo, lakini Kilichoniacha Mdomo wazi huku nikishika Kichwa kwa mshangao mkubwa, Ni baada ya Uongozi wa Timu hiyo kumchukua Kocha Denis Kitambi, kama Kocha Msaidizi wa Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara akisaidiana na Geoge ‘Best’ Nsimbe.

Sitaki kusema kuwa Kitambi sio kocha mzuri, Lakini kiuharisia pamoja na Malengo waliyonayo Azam FC, hawakupaswa kumchukua Kitambi kama Kocha wao kwa muda huu ambao wao wanasaka mafanikio makubwa Tanzania na Barani Afrika kwa Ujumla.

Oktoba 20 mwaka jana, Denis Kitambi, alitimuliwa kazi na Ndanda FC, licha ya kuipandisha Ligi kuu lakini akashindwa kuiongoza vyema, Kocha huyo alifanikwa kucheza michezo Mnne tu ya ligi kuu akifanikiwa kuibuka na ushindi mmoja dhidi ya Standi United kwa bao 4-1, na kuambulia kipigo mfululizo kutoka kwa Mtibwa bao 3-1, Coastal Unio 1-0 na Ruvu Shooting 3-1, kitu ambacho hakikuweza kuvumiliwa na Viongozi wa Ndanda na kuamua kumuachisha kazi.

Amekaa zaidi ya miezi mnne akiwa hana timu ya kufundisha hata ligi za mchangani, badala yake akahamia kwenye Uchambuzi wa Soka kupitia Runinga hadi hivi juzi Azam wanatangaza kuwa atakuwa katika benchi la Ufundi la timu hiyo ambayo inamarengo ya kufika mbali katika Soka la Afrika.
Najiuliza sana sipati jibu, Ni kigezo kipi kilichopelekea Azam kumuamini Denis Kitambi hadi kumpa Ukocha, Je. Ni kule kuchambua kwake michezo kupitia Azam TV? Lakini hapana kama ni uchambuzi tu mbona hata Kaka Edo Kumwembe anachambua tena zaidi!!, Ok nadhani wamemchukua kwasababu hana uchembe chembe wa Uyanga na Simba. Lakini!! Mbona Hata David Mwamaja hana itikadi hizo na bado ni bonge la Kocha?. Nimepata jibu, ‘KUJUA NDIO MPANGO’.

Nilichotegemea baada ya Omog kutimuliwa.

Omog bado alikuwa ni kocha mwenye uwezo mzuri tena mwenye uzoefu mkubwa, Hivyo basi kama kweli Uongozi uliridhia aondoke baada ya kushindwa kutimiza malengo, Nilitegemea kuwaona makocha wenye kiwango cha hari ya juu hata mara mbili ya Omog ili kuendeleza pale alipokwamia Mcameroon huyo na sio kutafuta mwalimu ambaye atashindwa hata kufunga kamba za viatu vya kocha aliyeondoka.

Awali kulikuwepo na Tetesi kuwa Azam wangemchukua Kocha wa Timu ya Taifa ya Nigeria Stephen Kesh, baada ya kiongozi mkubwa wa klabu hiyo kusema kuwa wapo kwenye mazungumzo mazuri na kocha huyo.

George ‘Best’ Nsimbe ni kocha mzuri sana na anauzoefa sana na timu za ukanda wetu wa Afrika Mashariki, Kama tunavyojua Timu za Kiarabu na Kutoka ukanda wa Magharibi ndio zimekuwa Sumu kwa Vilabu vya Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa, Hivyo angetafutwa Kocha labda kutoka Ukanda huo ili kuongezea nguvu kwa Nsimbe.

Hakuna mtu anae kataa kwamba Azam FC sio timu Tajili hapa Tanzania, na imefanikiwa kuleta upinzani mkubwa katika Soka la letu, Lakini kuna vitu ambavyo vipo ndani ya Uongozi na timu nzima ambavyo ndio vinaiangusha Azam FC ambavyo moja wapo ni Kufanya kazi kwa kujuana na kama wasipochangamka, kutimiza Ndoto itakuwa Wimbo.

Yote kwa yote mimi nimalizie tu kwa kusema kuwa “Azam FC Kitambi kuwa kocha msaidizi mmechemka tena sio kidogo” HUO NDIO UKWELI.

MWISHO.

No comments: