maelfu ya Watanzania wakiamini kwamba, kifo cha aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni John Damiano Komba ndiyo kile kilichotabiriwa na mnajimu Maalim Hassan Hussein Yahya, mwenyewe ameibuka na kusema sicho!
Akizungumza na Risasi Jumamosi katikati ya wiki hii jijini Dar, Maalim Hassan alisema kuwa, baada ya kifo cha Kapteni Komba ambaye alikuwa pia mwanasiasa mkubwa nchini, wengi wameamini utabiri wake alioutoa mwanzoni mwa mwaka huu kwamba kuna mtu maarufu mwanasiasa atafariki dunia ghafla, basi ndiye Komba.
“Kwanza nataka watu wajue siyo Komba. Yule mwanasiasa niliyemtabiria mimi yuko palepale. Yeye ataanguka jukwaani na atafariki papo hapo,” alisema Maalim.
Aliongeza kuwa, kifo cha Komba ni upepo wa mauti tu lakini hayumo katika matukio ya utabiri wake wa mwaka 2015 ambapo alichambua vizuri hali ya kisiasa nchini. Katika utabiri wake huo, Maalim Hassan alisema mwanasiasa huyo atakuwa mgombea wa urais (hakumtaja jina lake wala la chama) ambapo atapatwa na mauti hayo akiwa anahutubia jukwaani kwa ajili ya kampeni.
Kwa madai hayo, wengi walisema ni Komba kwa sababu katika kipindi cha kifo chake alikuwa anajiandaa na kampeni za ubunge jimboni mwake na pia alikuwa anajiandaa na nyimbo za kampeni za kuhamasisha upigaji kura mwaka huu.

No comments:
Post a Comment