Kim Jong-Un apeleka poda jeshini - LEKULE

Breaking

10 Mar 2015

Kim Jong-Un apeleka poda jeshini


Kiongozi wa kidikteta wa Korea Kusini Kim Jong-Un amejaribu kuonesha namna anavyojali masuala ya kijinsia kwa kuwapelekea askari wa kike poda za kujipodolea ,katika kambia ya kijeshi ya ndege za mashambulizi ya anga aliyoitembelea wakati dunia ikiadhimisha kilele cha siku ya wanawake duniani.

Kiongozi huyo wa kipekee asiyetabirika alituma salamu zake za pongezi kwa wake wa askari wa kikosi cha anga katika sherehe za wanawake ulimwenguni na kusherehekea mafanikio na mchango wa wanawake popote, wakati alipokitembelea kikosi cha siri cha anga na kukagua nguvu za kituo hicho kipya.

Kwa muujibu wa taarifa za ziara yake, kiongozi huyo hakukutana ana kwa ana na mwanamke yeyote lakini aliwataka maafisa wake kukabidhi chakula alichowapelekea askari wake ikiwemo vipodozi alivyowapelekea wanawake walioko katika jeshi hilo kama zawadi.

Kiongozi mkuu Kim alijieleza kama balozi wa nishati ya kijanai na kueleza nia ya kutumia nguvu ya upepo,sola na hata nishati kwa ujumla ili kukwamua tatizo la umeme nchini mwake ambako umeme umekuwa ukikatika katika kila uchao.

Wakati akifanya ukaguzi huo katika ziara hiyo hakusita kumsifu baba yake Kim Jong-ill,kwakumwelezea kuwa alikuwa mwenye Imani,mzalendo,aliyepambana na ubeberu wa kielimu na maadili ya kielimu.

Kim yeye mwenyewe alisoma mjini Geneva inaaminika kuwa ana miaka 32, alipiga picha ya pamoja na marubani wake ,huku akiwataka wawe tayari wakati wowote na kuwakumbusha kauli mbiu yao ya kusubiri amri ya chama ili kutekeleza mipango yao.

Ziara hiyo pia imechukuliwa kama ziara ya mafunzo,huku vifaa mbali mbali vikigawiwa kama vyoo,vifaa vya kulia,vifaa vya jikoni,mahema ya uzalishaji mazao na zana za chumba cha kuzalishia uyoga.

Msafara wake ulielekea katika kituo hicho kwa kutumia ndege yake binafsi ya Soviet-era IIyushin Il-62.

No comments: