Serikali ya Kenya imeutambua rasmi mwili wa jamaa mmoja uliopatikana katika mbuga ya wanyama, kuwa ni wa shahidi wa mahakama ya ICC, Meshack Yebei, katika kesi inayomkabili makamu wa rais wa Kenya, William Ruto.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, uchunguzi wa chembechembe za DNA umehakikisha fika kuwa ni yeye.
Tangazo hilo linatarajiwa kuipa afueni familia ya Yebei, ambayo nusura izike mwili tofauti mnamo mwezi Januari, kabla ya kuambia kwamba mwili huo haukuwa wa mtoto wao.
Mwanachemia wa serikali ya Kenya hatimaye ametangaza kuwa mwili Fulani ambao umelala kwenye chumba cha kuhifadhia maiti tangu mwezi Desemba ni wa Meshack Yebei.
Bwana Yebei alitarajiwa kuwa shahidi wa mshtakiwa kwenye kesi dhidi ya Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji katika mahakama hiyo ya kimataifa huko Hague.
Gazeti moja la Kenya limemnukuu afisa wa uchunguzi akisema kwamba chembechembe za DNA zimedhibitisha kwamba mwili huo uliopatikana ni wa Yebei.
Matokeo haya ni sambamba na yale yaliyochapishwa na daktari mmoja wa Afrika Kusini aliyepewa kazi hiyo na familia.
Inatarajiwa kuwa serikali sasa itafanya uchunguzi wa pili kugundua kilichosababisha kifo chake.
Inasemekana kwamba Meshack Yebei alitekwa nyara mwishoni mwa mwezi Desemba nyumbani kwake Eldoret alipokwenda kumwona mkewe ambaye alikuwa anaugua.
ICC imefichua kuwa marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi na makazi salama lakini akakataa.
Mwezi Januari mwili ulioharibika vibaya ulipatikana katika mto ulio takriban kilomita arobaini kutoka nyumbani kwake, na familia ikadhani kuwa ni yeye.
ICC imefichua kuwa marehemu alipewa nafasi ya kupata u
Lakini uchunguzi wa DNA ukaonyesha kuwa ni mwili wa mtu mwengine ambaye pia alitoweka wakati huo huo.
Kufikia wakati huo familia yake tayari ilikuwa inalalamika kuwa kutoweka kwake Yebei kunatokana na kuhusishwa na kesi hiyo nyeti.
Ufumbuzi huu sasa unaibua maswali mapya.
Mbuga ya Wanyama ya Tsavo, ambako mwili huo ulipatikana, iko takriban kilomota mia sita kusini mashariki mwa Eldoret alikotoweka.
Aidha familia yake imelalamika kuhusu muda ambao serikali imechukua kutangaza matokeo ya DNA, na imetishia kuuchukua mwili huo ili iuzike wiki hii, iwapo serikali itatoa thibitisho hilo au la.
No comments:
Post a Comment