Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea mkoani Ruvuma ambako alihudhuria mazishi ya Kada wa CCM na Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi Marehemu John Damiano Komba aliyefariki hivi karibuni, Chama cha Mapinduzi kilikuwa na maombolezo ya kitaifa ya siku tatu mpaka mazishi ya kiongozi huyo yalipofanyika jana yakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete.
Ndugu Abdulrahman Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma akianzia wilaya ya Mpwapwa kabla ya kuendelea na ziara hiyo katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Ndugu Adam Kimbisa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Ndugu Mwigulu Nchema.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanaCCM na wananchi waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akiongozana na viongozi wenzake mara baada ya kuwasili mjini Dodoma kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Kapteni Chiku Galawa, Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, na Adam Kimbisa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili mjini Mpwapwa ambako ndiko ameanzia ziara yake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Dr. Jasmine Tisekwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Mpwapwa katika ofisi ya CCM wilaya ya Mpwapwa kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati alipokuwa akisalimia wananchi mjini Mpwapwa, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment