Je, Rais Kikwete Amevunja Katiba Kuteua Wabunge Wawili Kwa Muda Huu Uliosalia?......Mwanasheria Mkuu wa Serikali Amelijibu Swali. - LEKULE

Breaking

27 Mar 2015

Je, Rais Kikwete Amevunja Katiba Kuteua Wabunge Wawili Kwa Muda Huu Uliosalia?......Mwanasheria Mkuu wa Serikali Amelijibu Swali.

Mwanasheria mkuu wa Serikali, Mh. George Masaju  amesema  leo  Bungeni  kuwa Katiba  haikuvunjwa  kwa  Rais  Kikwete  Kuteua  wabunge  Wawili, miezi  mitatu  kabla  ya  Bunge  la  Kumi  halijavunjwa.

Masaju  aliyasema  hayo  wakati  akijibu mwongozo  ulioombwa  na   Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma Bw. Felix Mkosamali.

Akijibu  hoja  ya  kiinua  mgongo  kwa  wabunge  hawa  wapya, Spika  wa  bunge  amesema  kuwa  malipo  hayo  yanategemea  na  siku  watakazofanya  kazi  na  kwamba  hayawezi  kuwa  sawa  na  wabunge  wengine.


No comments: