Je, historia ya mwaka 2005 itajirudia? - LEKULE

Breaking

9 Mar 2015

Je, historia ya mwaka 2005 itajirudia?



Wababe wa ligi kuu England Manchester United na Arsenal leo wanavaana katika uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa robo fainali za mashindano ya FA Cup huku mashabiki wa soka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi walioupata vijana wa mzee Wenger mwaka 2005, kutoka mikononi mwa wapinzani wao hao wakubwa wajulikanao kama Mashetani wekundu. Katika mpambano huo wa fainali uliofanyika katika dimba la Millenium Studiuma, Arsenal waliibuka washindi kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 120 za kipute hicho bila kufungana. Timu zote mbili zimekwishabeba kombe hilo mara 11. Ni kweli FA Cup si lolote? Bosi wa Manchester Utd Louis van Gaal amesema kuwa kumaliza ligi huku ukiwa katika nne bora ni jambo la muhimu sana kwake yeye kuliko hata kuishinda kombe la FA. Kauli ya kocha huyo inakuja huku kukiwa imebaki saa kadhaa kwa Manchester Utd kuvaana na wapinzani wao wa muda mrefu Arsenal. ‘’Kumaliza katika nafasi nne za mwanzo ni matokeo bora na kwa sisi Manchester Utd nafikir ni bora zaidi’’ alisema Van Gaal. ‘’Kama unashinda kombe la FA huingii katika mashindano ya klabu bingwa lakini ndo umekuwa bingwa’’ aliongeza. Manchester Utd inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya England kwakuwa na point 53 ikitofautiana point moja tu na wapinzani wao Arsenal iliyo nafasi ya tatu wakiwa na point 54, huku nafasi ya tano ikishikwa na Liverpool yenye point 51.

No comments: