'I am Happy' Pharrell taabani tena - LEKULE

Breaking

16 Mar 2015

'I am Happy' Pharrell taabani tena


Mwimbaji Pharell Williams sasa anashtumiwa na familia ya Marvin Gaye kwa kuiba utunzi wa gwiji huyo katika wimbo wake maarufu ''Happy''
Lakini wapenzi wa muziki wa kufoka anaouimba Pharell wameanza kujiuliza maswali mengi tu, kuhusiana na familia ya marehemu Marvin Gaye .
Familia hiyo ilipokea takriban dola milioni 7.3 majuzi tu kutokana na uamuzi wa mahakama uliompata Pharell kwa ushirikiano na Robin Thicke na hatia ya kunakili bila idhini utunzi wa Gaye wa mwaka wa 1977 '' Got To Give It Up''
Na Sasa wameanza tena kumulika kurunzi yao kwa wimbo uliovuma wa ''Happy ''

Yamkni mwanawe marehemu Gaye, Nona anasema wako na ushahidi wa kutosha wa kudhibitisha kuwa wimbo huo unaigiza wimbo wa mwaka 1966'' Ain't That Peculiar''.
Mkewe wa awali ,Janis alisikika akisema "Nimesikia wimbo huo mdundo wake na jinsi ala zilivyopangwa na sina haja ya kujibizana unajua vyema kuwa nimeusikia wimbo wa happy na vilevile mimi ninaujua '' Ain't That Peculiar''
Kwa sasa sina mambo mengi ya kusema '' Alisema Janis.
Mahakama nchini Marekani ilitoa hukumu juu ya wimbo bora katika mauzo uitwao Got To Give it Up.

Hukumu hiyo imetolewa dhidi ya wanamuziki Robin Thicke na Pharrell Williams walionakili wimbo huo.
Katika hukumu hiyo mahakama moja ya mjini Los Angeles iliamuru kuwa wimbo wa Blurred Line ' ulioimbwa kwa ushirikiano kati ya Robin Thick na Pharrell Williams kwa kosa la kunakili wimbo wa Marvin Gaye uliowahi kutamba mwaka 1977 uitwao Got To Give It Up'.
Wanamuziki hao wawili walihukumiwa kulipa dola za kimarekani zaidi ya milioni saba kama fidia kwa familia ya marehemu Marvin Gaye.

No comments: