FIFA:Algeria ni timu bora Afrika - LEKULE

Breaking

13 Mar 2015

FIFA:Algeria ni timu bora Afrika


Algeria imesalia timu bora barani Afrika katika orodha ya FIFA ya mwezi March licha ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha kombe la mataifa bingwa ya Afrika na Ivory Coast.

''The Desert Foxes'' walitupwa nje ya mashindano hayo na The Elephants ya Ivory Coast katika hatua ya robo fainali.

Hata hivyo ushindi huo wa ''The Elephants'' huko Equatorial Guinea, mabingwa hao waliwapiku kwenye orodha hiyo mpya iliyotolewa Alhamisi.

Algeria wameorodheshwa katika nafasi ya 18 duniani huku Ivory Coast ikiorodheshwa ya 20 duniani .

Black stars ya Ghana ni timu ya tatu kwa ubora barani lakini imeorodheshwa katika nafasi ya 24 duniani.

Tunisia ni ya nne barani Afrika lakini ya 25 duniani.

Senegal inafunga orodha ya tano bora barani Afrika.

Timu hiyo hata hivyo imeorodheshwa katika nafasi ya 36 duniani.

Kwa mara ya Kwanza wenyeji wa kombe la mataifa bingwa ya Afrika Equatorial Guinea wameondolewa katika nafasi kumi bora barani afrika licha ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye kipute hicho cha mwaka huu.

Orodha ya nafasi kumi bora barani Afrika.

1 (18). Algeria

2 (20). Ivory Coast

3 (24). Ghana

4 (25). Tunisia

5 (36). Senegal

6 (38). Cape Verde

7 (41). Nigeria

8 (44). Guinea

9 (47). DR Congo

10 (49). Cameroon

No comments: