FA:Cisse na Evans kutocheza mechi 7 - LEKULE

Breaking

7 Mar 2015

FA:Cisse na Evans kutocheza mechi 7


Shirikisho la Soka nchini Uingereza FA limewapiga marufuku wachezaji Jonny Evans wa Manchester United na Papiss Cisse wa Newcastle kutocheza mechi saba kwa kutemeana mate.

Evans mwenye umri wa miaka 27 alikuwa amekana mashtaka ya kumtemea mate Cisse katika mechi dhidi ya Manchester ambapo kilabu hiyo ya Old Trafford iliibuka mshindi kwa 1-0

Bwana Evans alipinga madai hayo lakini yakabainishwa,ilisema taarifa ya FA.

Cisse mwenye umri wa miaka 29 alikubali mashtaka aliyowekewa na sasa amepigwa marufuku kwa mechi nane kwa kuwa tayari alikuwa amehudumia marufuku msimu huu.

No comments: