MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ametoa siku saba kwa uongozi wa Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kuacha kutiririsha maji taka kwenyenda barabarani na kwenye makazi ya watu.
Agizo hilo amelitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushitukiza ya kukagua barabara, madaraja na miundombinu eneo la Msasani ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hasa wakati wa mvua za masika.
"Natoa siku saba kwa uongozi wa Hospitali ya TMJ kuhakikisha wanaacha kutiririsha maji taka kutoka katika hospitali hiyo kinyumbe cha agizo langu zitafuata hatua kali za kisheria" alisema Makonda.
Katika hatua nyingine Makonda aliwataka wakazi wa eneo hilo la Msasani kuacha kutupa takataka kwenye mitaro ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa kuziba kwa mitaro hiyo na kuwa mtu yeyote atakayebainika akitupa taka taka hizo atachukuliwa hatua kali.
Makonda alisema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kujenga na kutengeneza barabara lakini watu wachache wamekuwa wakiharibu kwa kutupa taka taka hovyo.
No comments:
Post a Comment