Dar es Salaam
Partly cloudy conditions and
35°C/25°C
Jobs
ASSISTANT ACCOUNTANT
Private Agricultural Sector Support (PASS) Trust
Deadline: Mar 13, 2015
Post for Free
View All
HABARI KUU LEO
Mar 3, 2015
Komba
JOHN
Kikwete
Katiba
MBEYA
Ndoa
Dar Es Salaam
Marekani
CCM
Mapenzi
Yanga
Tanzanian
Malaysia
UINGEREZA
Arusha
Zanzibar
Mwanza
YANGA
Marekani
Wema
POPULAR ON YOUTUBE
Bakhresa, Mo Dewji ni zaidi ya dhahabu
TANZANIA inaingiza fedha nyingi za kigeni kupitia wafanyabiashara wawili; Said Bakhresa na Mohamed Dewji kuliko fedha inazoingiza kupitia mauzo ya dhahabu nje ya nchi, imefahamika.Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu, alisema jijini Dar es Salaam juzi Jumatatu kwamba kiasi cha fedha za kigeni zinazoingizwa na madini ya dhahabu kimeshuka kwa mwaka uliopita.Katika mada yake iliyoitwa The Importance of Economic Transformation (Umuhimu wa Mabadiliko ya Kiuchumi), Profesa Ndullu alieleza kwamba wakati miaka michache iliyopita dhahabu ilikuwa ikiongoza kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni, hivi sasa inazidiwa na sekta ya utalii na viwanda (uzalishaji).Katika mchanganuo huo wa mapato, utalii uliingiza dola bilioni mbili, viwanda dola bilioni 1.4 (shilingi trilioni 2.5) na dhahabu dola bilioni 1.2 (shilingi trilioni 2.1). Sekta ya Usafirishaji hususani bandari ililiingizia taifa kiasi cha dola milioni 800 huku kilimo kikiingiza dola milioni 700.Kwa mchanganuo huo wa Ndullu, bandari peke yake imeingiza fedha nyingi za kigeni kuliko sekta ya kilimo ambayo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa.“Tusitegemee kilimo kuondoa umasikini kwani umuhimu wa kilimo kwenye kuingiza fedha za kigeni unaonekana kupungua. Kitakwimu, mchango wa kilimo kwenye Pato la Taifa ulikuwa asilimia 30 mwaka 1998 wakati mwaka 2013 ulikuwa ni asilimia 21.Hata hivyo, ni lazima kwanza kabisa kuendelea kuwekeza kwenye kilimo ili kupunguza tofauti ya kipato miongoni mwa wananchi kwani bado kilimo kinaajiri asilimia 70 ya Watanzania,” alisema Ndullu katika mkutano wa kiuchumi uliofanyika jijini Dar es Salaam.Kilimo kinaonekana kutofanya vizuri katika miaka ya karibuni, kwa vile ripoti hiyo ya Ndullu imeonyesha kushuka kwa kiwango cha fedha za kigeni kinachotokana na mazao ya asili ya biashara kama pamba na kahawa kushuka thamani huku korosho pekee ndiyo ikionekana kupanda.Bei ya dhahabu imeshuka katika soko la dunia na kwa mujibu wa Profesa Ndullu, hiyo inaweza kuwa sababu mojawapo ya kushuka kwa mapato ya fedha za kigeni kwa bidhaa hiyo.Kwa mujibu wa mada hiyo ya Ndullu, fedha hizo za kigeni zinazoingia Tanzania zinatokana na mauzo ya bidhaa kama nyuzi na vitambaa, nyuzi za katani na magunia, saruji na unga ( ngano na sembe).Nyingi ya bidhaa hizo hutengenezwa hapa nchini katika viwanda vinavyomilikiwa na wafanyabiashara wawili matajiri hapa nchini; Mohamed Enterprises cha Dewji na vile vya Azam vilivyo chini ya biashara za Bakhresa.Ujio wa tajiri namba moja barani Afrika, Aliko Dangote, katika sekta ya uzalishaji saruji unaweza kuongeza zaidi mapato ya sekta hiyo na fedha za kigeni pia.Ingawa mada hiyo ya Profesa Ndullu haikutaja mgawanyiko wa kiasi hicho cha shilingi trilioni 2.5, ripoti za miaka ya nyuma za BoT zimeyataja makampuni ya Bakhresa na MeTL kama vinara wa uzalishaji hapa nchini.Katika ripoti za karibuni za majarida ya kimataifa kama Forbes la Marekani, majina ya Bakhresa na Dewji yamekuwa yakitajwa kama miongoni mwa Watanzania matajiri zaidi.
No comments:
Post a Comment