Apple yaipiku Samsung kwa mauzo - LEKULE

Breaking

5 Mar 2015

Apple yaipiku Samsung kwa mauzo

Kampuni ya Apple iliuza simu nyingi zaidi aina ya Smartphone katika robo ya mwisho ya mwaka na kuishinda kampuni ya kielektroniki ya Samsung kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011 baada ya utumizi wake wa simu za iphone zenye vioo vikubwa kupata umaarufu kulingana na data iliopatikana na Gartner.

Apple iliuza simu millioni 74.8 katika mgao wa soko wa asilimi 20.4 huku Samsung ikiuza simu millioni 73 katika mgao wa soko wa asilimia 19.9 ya robo ya mwisho ya mwaka 2013.

Apple iliikaribia Samsung kwa mauzo millioni 50.2 katika soko lenye his asilimia 17.8 ikilinganishwa na Samsung iliouza simu millioni 83.3 na asilimia 29.5 ya hisa.

Mauzo ya Samsung yalishuka katika soko la simu aina ya Smartphone katika robo ya nne ya mwaka 2014 ,wakati ilipopoteza karibia asilimia 10 ya alama katika soko hilo kulingana na Anshul Gupta ambaye ni mtafiti mkuu na mchanganuzi wa Gartner.

Hisa za Sumsung ambazo zilikuwa zimepanda katika robo ya tatu ya mwaka 2013,zimepokea shinikizo kali huku kampuni hiyo ikibanwa katikati ya Apple pamoja na wafanyibiashara wa Uchina.

Robert ambaye ni mkurugenzi wa maswala ya utafiti amesisitiza kuwa Samsung itahitaji kubuni programu mpya pamoja na huduma tofauti ili kuinua mauzo yake.

Wikendi iliopita Samsung ilizindua simu ya Galaxy 6 ambayo ina kioo kilichojipinda pamoja na mfumo mpya wa malipo.

No comments: