Andy Murry kuuaga ukapera - LEKULE

Breaking

20 Mar 2015

Andy Murry kuuaga ukapera

Ni mwaka wenye hadhi na uzito kwa mcheza tennis Andy Murray, hali hiyo si tu kutokana na matumaini yake ya kuongeza taji la pili la Grand Slam bali ni mpango alionao wa kufunga ndoa na mpenzi wake Kim Sears April mwaka huu.
Mchezaji huyo raia wa Scotland amerejea katika nafasi ya nne duniani baada ya awali kuporomoka kutokana na upasuaji wa mgongo aliofanyiwa.
Furaha ya mchezaji huyo inachagizwa zaidi kutokana na rekodi mpya aliyojiwekea baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali katika mashindano ya Indian Wells yanayoendelea huko California Marekani.

No comments: