wakaazi waliolazimika kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani katika eneo la Maiduguri nchini Nigeria
Jeshi la Nigeria limesema kuwa
limefaulu kusambaratisha shambulio la pili la Boko Haram, juma moja tu
baada ya kusambaratisha jaribio jingine la mashambulizi katika eneo la
kazkazini mashariki mwa Maiduguri.
Msemaji wa jeshi Meja Jenerali
Chris Olukade, amesema kuwa waliwauwa waasi wengi wa Boko Haram katika
shambulio hilo la hivi punde, huku wakipata bunduki, risasi na magari
yaliyokuwa yakitumika na waasi hao wa Boko Haram.
No comments:
Post a Comment