Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam,jana iligeuka mithili ya
uwanja wa sinema baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kuwafutia
mashitaka watu 30 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Wananchi
(CUF) kutimua mbio na kutoweka eneo la mahakama hiyo.
Kitendo
hicho kiliwafanya wafuasi hao wanusurike kuunganishwa katika kesi
inayomkabili Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, katika mahakama
hiyo.
Tukio
hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi baada ya upande wa Jamhuri
ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, Mawakili wa
Serikali, Joseph Maugo na Mwanaamina Kombakono, kudai kuwa DPP
amewasilisha hati ya kuwafutia kesi washtakiwa na hivyo, hana nia ya
kuendelea kuwashitaki.
Alidai DPP analiondoa shauri hilo chini ya kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Sheria za Makosa ya Jinai (CPA).
Hakimu
Mchauru alisema kwa kuwa DPP ameona hana nia ya kuendelea kuwashitaki,
mahakama yake haina sababu ya kuendeleaa kuwashikilia washtakiwa, hivyo
inawaachia huru.
Baada ya washtakiwa hao kuachiwa huru walitoka eneo la mahakama na kutimua mbio wakiwa sambamba na wadhamini wao.
Saa
5:10 asubuhi, mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mchauru,
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba alipanda kizimbani kusikiliza kesi
yake.
Jopo
la mawakili wa serikali liliomba mahakama kubadilisha hati ya mashitaka
na kuwaunganisha wafuasi 30 pamoja na Profesa Lipumba, wakati huo
wakiwa wamekwishaondoka katika eneo la mahakama na kutawanyika.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 23, itakapotajwa tena wakati washtakiwa wote wakiwa nje kwa dhamana.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 23, itakapotajwa tena wakati washtakiwa wote wakiwa nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment