Aliyekuwa mwimbaji muziki wa gospel na baadaye kurudi kwenye Bongo
Fleva,Stara Thomas amekana habari zilizoenea hivi karibuni kuwa
amefumaniwa na mpenzi wake nyumbani kwake.
Akizungumza na Soudy Brown kupitia Uheard alisema kuwa mwanamke kama
yeye hawezi kufumaniwa na kwamba mpenzi wake wa sasa kinachomsumbua ni
wivu wa kimapenzi bila kumtaja jina mpenzi wake huyo wa sasa.
Aidha
ameongeza kuwa hayuko tayari kuzungumzia suala hilo kwa sasa ndiyo maana
amekaa kimya tangu habari hizo zitoke kwenye magazeti.
‘’Nimeamua kunyamaza kimya lakini ipo siku ntazungumza kila kitu kuhusiana na habari hizi," alisema Stara.
No comments:
Post a Comment