Robert Mugabe afikisha miaka 91 - LEKULE

Breaking

22 Feb 2015

Robert Mugabe afikisha miaka 91


 Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimia miaka 91 leo.

Yeye sasa ni kiongozi mzee kabisa duniani, na amekuwa madarakani kwa miaka 35.

Sherehe ya siku yake ya kuzaliwa itafanywa juma lijalo.

Anatarajiwa kufanya sherehe kubwa katika uwanja wa golf huko Victoria Falls, inakisiwa sherehe yenyewe itagharimu dola milioni moja.

Maelfu ya watu watahudhuria karamu hiyo, ambapo kutachinjwa ndovu, nyati, paa na simba mmoja.

Shirika la habari la taifa linasema wananchi watalipia dhifa hiyo

Zimbabwe ni moja kati ya nchi maskini duniani.

No comments: