Wakala
wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), unategemea kuanza rasmi mkakati
wa kuwasajili na kuwapa vyeti vya kuzaliwa wanafunzi wa shule za msingi
za Manispaa ya Kinondoni na mpango huo utatekelezwa katika takribani
shule 140 zenye wanafunzi wapatao 155,944.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kitengo cha
mawasiliano cha wakala huyo, lengo la usajili huo katika awamu hiyo ni
kusajili wanafunzi 20,000.
Ilisema
kuzinduliwa kwa mkakati huo katika Manispaa ya Kinondoni ni muendelezo
wa mkakati mkuu uliozinduliwa Aprili, mwaka jana unaowawezesha wanafunzi
wa Shule za Msingi na Sekondari kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa
katika shule wanazosoma.
Taarifa
ilisema baada ya mwalimu kuwatangazia wanafunzi na wazazi kuhusu huduma
hiyo kupatikana shuleni atagawa fomu za maombi kwa wanaohitaji,
kuhakiki fomu zilizojazwa, kuzikusanya na kuziwasilisha RITA kwa ajili
ya kuhakiki na kuandaliwa vyeti.
Tayari
mkakati huo umeshaanza kutekelezwa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar
es Salaam na umeshafanyika katika shule 105 za msingi na 96 za sekondari
za Manispaa ya Ilala na kuonesha mafanikio ambapo zaidi ya wanafunzi
16,000 wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.
No comments:
Post a Comment