Red Arrow FC kuweka kambi Tanzania - LEKULE

Breaking

13 Feb 2015

Red Arrow FC kuweka kambi Tanzania


Klabu ya Red Arrow FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia inatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam-Tanzania jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya kuweka kambi ya mafunzo ya wiki moja kujindaa na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo 2015.

Uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake Col Nolacso K Chilando ulifika makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF sambamba na Afisa habari wa klabu Lt Col Melody Siisii, Bw Alex Chila ofisa ubalozi wa Zambia nchini Tanzania kujitambulisha uwepo wao nchini.

Wakiongea na katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF Selestine Mwesigwa, uongozi wa timu hiyo umesema maandalizi ya kambi yamekamilika na kikubwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania watambue uwepo wao na kuwasaidia kupata viwanja vya kufanyia mazoezi.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF Mwesigwa alisema wameyapokea maombi hayo ya Red Arrow FC na kuwakaribisha nchini kwa ajili ya kambi yao na kusema ujio wao utafungua milango kwa vilabu vingine pia kuweka kambi Tanzania.

Timu ya Red Arrow FC inayomilikiwa na jeshi la Anga nchini Zambia ikiwa nchini kwa mafunzo, inatarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na imeliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania kuwatafutia timu moja ya kucheza nayo.

No comments: