Rais Kikwete apokea vitabu Mil 2.5 vya Sayansi - LEKULE

Breaking

25 Feb 2015

Rais Kikwete apokea vitabu Mil 2.5 vya Sayansi


Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya elimu hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha vijana wanaosoma katika shule za sekondari wanapata elimu bora mara kabla ya kuhitimu.
 
Rais Kikwete aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea vitabu milioni 2 na laki 5 vya masomo ya Sayansi na Hisabati kutoka serikakali ya Marekani kupitia balozi wake hapa nchini Bw. Mark Childress.
 
Alisema kupitia vitabu hivyo vimesaidia kupunguza uhaba wa vitabu uliokuwepo katika shule za sekodari kutoka uwiano wa watoto watano kusoma kitabu kimoja na kufikia watoto mtoto mmoja kusoma kitabu kimoja kwa sasa.
 
Aidha Rais Kikwete amezitaka taasisi za serikali kutumia majeshi yaliyopo katika kusafirisha vitu vya serikali kama ilivyofanywa na ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI katika kusafirisha vitabu hivyo na kuvipeleka katika kila mkoa kwa kuwa kufanya hivyo kutaondoa uwezekano wa vitendo vya rushwa iwapo kama tenda hiyo ingetangazwa kwa lengo la kupata mzabuni
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,na viongozi wengine wakiangalia jinsi somo la sayansi likifundishwa katika darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,na viongozi wengine wakisalimia wanafunzi katika darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, wakiongea na mkandarasi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyotolewa na Watu wa Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam wakiwa na vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam wakiimba kwa furaha katika sherehe ya kukabidhiwa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani
Kikundi cha utamaduni cha jeshi la polisi kikitumbuiza katika sherehe ya kukabidhiwa vitabu vya sayansi vilivyotolewa na Watu wa Marekani

No comments: