Mwanamke Anyongwa hadi Kufa na Mpenzi wake Usiku wa Manane Wakiwa Gesti - LEKULE

Breaking

24 Feb 2015

Mwanamke Anyongwa hadi Kufa na Mpenzi wake Usiku wa Manane Wakiwa Gesti

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia, Erick Bruno (30) kwa tuhuma za kumnyonga hadi kufa mpenzi wake, Daja Dungu (35) wakati walipokuwa kwenye nyumba ya kulala wageni (jina tunalo) Manispaa ya Morogoro.

Akizungumzia kutokea kwa tukio hlo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul, alisema tukio hilo lilitokea Februari 23, mwaka huu saa 6.30 usiku katika karakana ya Kichangani ambapo mtuhumiwa alikodisha chumba namba nane, akiwa na na mwanamke huyo.

“Februari 23, mwaka huu saa sita na nusu mtuhumiwa alifika kwenye nyumba hiyo akiwa ameambatana na huyo mwanamke kwa lengo la kufanya ngono baada ya muda kukasikika kelele za kuomba msaada,” alisema Paulo.

Paulo alisema baada ya kelele hizo mlinzi wa nyumba hiyo aliwaita watu na kumtaka mtuhumiwa afungue mlango, lakini alikataa kwa kudai kuwa hakuna kitu kilichotokea, ndipo juhudi za kuufungua mlango zilifanyika na kumkuta mwanamke huyo akiwa amefariki.

Aidha, Paulo alisema Polisi bado haijafanikiwa kupata chanzo cha tukio hilo na kuwa upelelezi unafanyika ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.

Kamanda Paul, alisema mtuhumiwa anashikiliwa Polisi kwa upelelezi zaidi na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.

No comments: