Bw Simon Wambugu Gichamba akiwa kortini Nairobi Februari 27, 2015.
KILIO kilitanda katika mahakama ya Nairobi Ijumaa wakati mshukiwa wa mauaji ya Mbunge wa Kabete George Muchai alipodai ameteswa na kuhasiwa na maafisa wa polisi wanaomhoji.
Wazazi, jamaa na hata mkewe mshukiwa huyo walidodokwa na machozi waliposikia simulizi za Simon Wambugu Gichamba kwa hakimu mkazi Bi Miriam Mugure.
Gichamba hakujizuia ila alilia wakati wa kipindi chote kesi yake ilipokuwa inaendelea.
Wakili Amadi Shamalla alimweleza Bi Mugure kwamba mshukiwa aliteswa kinyama na hata “hakukubaliwa kumwona wakili wake.”
Bw Shamalla alisema mshukiwa huyo hakukubaliwa kutembelewa na jamaa zake.
“Wazazi wa mshtakiwa walienda kumtembelea mshtakiwa rumande lakini polisi hawakuwakubalia wamwone. Hata mimi sikukubaliwa kumwona,”akasema Bw Shamalla.
Wakili huyo alidokeza hata yeye alipoenda kumwona pia naye alinyimwa fursa ya kumwona.
“Mheshimiwa mshukiwa huyu amepigwa na kuteswa kinyama alipokuwa anahojiwa na maafisa wa polisi. Gichamba alipigwa na hata amehasiwa. Naomba hii mahakama iamuru mshukiwa huyu apelekwe hospitali,” wakili Shamalla alimweleza Bi Mugure.
Bw Shamalla aliomba mshukiwa apelekwe hospitali ama akubaliwe atibiwe na daktari wa kibinafsi.
“Naomba hii mahakama iamuru Gichamba apelekwe katika hospitali kuu ya Kenyatta kutibiwa. Ikiwa polisi hawatampeleka basi akubaliwe kutibiwa mara moja na daktari wa kibinafsi,” akarai Bw Shamalla.
Wakili huyo pia aliomba Gichamba aachiliwe kwa dhamana ikiwa polisi hawajakamilisha uchunguz
Bi Mugure aliamuru mshtakiwa apelekwe katika hospitali kuu ya Kenyatta kutibiwa na ripoti jinsi i.
Lakini kiongozi wa mashtaka Daniel Karori aliiambia mahakama kuwa uchunguzi haujakamilishwa.
Aliomba muda wa siku nyingine 10 ndipo maafisa wa upelelezi wakamilishe uchunguzi.
“Polisi hawajakamilisha uchunguzi wa kesi hii,” akasema Bw Karori na kuongeza, “ uchunguzi ukikamilishwa mshukiwa huyu ataunganishwa na washukiwa wengine watano wanaoendelea kuhojiwa. Wote watafunguliwa shtaka la mauaji ya Muchai.”
Washtakiwa wengine
Mahakama ilifahamishwa kwamba ikiwa mshukiwa atatibiwa na daktari wa kibinafsi atagharamia huduma hizo.
alivyoumizwa iwasilishwe mahakamani.
Hakimu aliamuru kesi hiyo itajwe tena Machi 10 ndipo upande wa mashtaka ueleze ikiwa maafisa wa polisi wamekamilisha uchunguzi.
Gichamba atashtakiwa pamoja Erick Muyera Isabwa kwa jina jingine Chairman, Raphael Kimani Gachihi (Kim), Mustafa Kimani Anyonyi (Musti), Stephen Asitiva Lipapo (Chokore) na Jane Wanjiru Kamau (Ciro).
Wote wanachunguzwa kwa makosa ya kumuua Muchai, walinzi wake wawili na dereva.
No comments:
Post a Comment