Misri yamhukumu mwandishi miaka 5 jela - LEKULE

Breaking

23 Feb 2015

Misri yamhukumu mwandishi miaka 5 jela

Mahakama moja mjini Cairo Misri imemhukumu mwandishi wa blogu kifungo cha miaka 5 jela kwa kukiuka sheria za undamanaji

Mahakama hiyo ilimpata na hatia mwanablogu Alaa Abdel Fattah, kwa mchango wake katika maandamano na mapinduzi ya serikali mwaka wa 2011.

Majaji walimpata na hatia ya kukiuka sheria zinazosimamia undamaji nchini humo.

Kauli hiyo ni kama msumari kwenye kidonda kwa Alaa Abdel Fattah ambaye alikuwa ameachiliwa kwa

dhamana na mahakama nyengine nchini mwaka uliopita baada ya kukata rufaa ya kifungo cha miaka 15 jela.

Alaa Abdel Fattah alijipatia sifa baada ya kuwa mstari wa mbele kupinga udhalimu uliokuwa ukiendelezwa na

utawala wa aliyekuwa rais wa muda mrefu nchini humo Hosni Mubarak.
Hii ilikuwa dalili mbaya kwa waandishi wa habari wa shirika la utangazaji la Al-Jazeera, Mohamed Fahmy na Baher Mohamed
ambao walirejea leo mahakamani kwa kusikizwa kwa kesi dhidi yao.
Hata hivyo kesi dhidi yao iliahirishwa hadi Machi tarehe 8 kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press

No comments: