Mfahamu mkimbiaji bora kwenye Epl . - LEKULE

Breaking

13 Feb 2015

Mfahamu mkimbiaji bora kwenye Epl .



Nyota wa klabu ya Manchester City James Milner ametajwa kuwa mchezaji aliyekimbia umbali mrefu kuliko wote kwenye ligi ya England ambapo ameweza kuvunja rekodi iliyowahi kuwekwa kwa mujibu wa tamwimu rasmi .

Milner amefanikiwa kukimbia umbali mrefu kwenye mchezo mmoja wa ligi kuu ya England kuliko mchezaji yoyote mwingine kwenye ligi kuu ya England katika mchezo kati ya timu yake na Stoke City kwenye uwanja wa Britania uliopigw ahapo jana (jumatano ).

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za EPL Milner alifanikiwa kukimbia umbali wa kilomita 13.56  umbali ambao ni rekodi ya umbali mrefu kuliko wowote ule uliowahi kurekodiwa kwa mechi za msimu huu wa ligi ya England .

Kiungo huyu mwenye umri wa miaka 29 ambaye amekuwa moja kati ya wachezaji wasiopewa sifa sana lakini ambaye siku zote anatimiza wajibu wake ipasavyo awapo uwanjani amekuwa kwenye kiwango kizuri katika mechi mbili zilizopita ambapo amefanikiwa kufunga mabao mawili mfululizo .

Kiungo wa Hull City George ndio mchezaji pekee ambaye ameweza kurekodiwa kuwa na takwmu ya kukimbia umbali mrefu mara nyingi kuliko mchezaji yoyote akiwa amefanya hivyo kwenye michezo dhidi ya Aston Villa ambapo alikimbia umbali wa km 13.24, dhidi ya Manchester United ambapo alikimbia umbali wa km 13.30, dhidi ya Stoke City na dhidi ya Newcastle ambako kote alikimbia zaidi ya umbali wa km 13.

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane na kiungo wa timu hiyo Christian Eriksen na kiungo wa Manchester United Marouanne Fellaini nao wameingia kwenye rodha ya wachezaji waliokimbia umbali mrefu kuliko wote .

WACHEZAJI WALIOKIMBIA UMBALI MREFU KWENYE MECHI ZA EPL MSIMU HUU.

James Milner – MAN CITY vs Stoke – 13.56km

George Boyd –  BURNLEY vs Newcastle – 13.55km

Tom Carroll –    SWANSEA vs Southampton – 13.47km

George Boyd –  BURNLEY vs Stoke – 13.34km

George Boyd –  BURNLEY vs Man Utd – 13.30km

George Boyd –  BURNLEY vs Aston Villa – 13.24km

Gylfi Sigurdsson – SWANSEA vs Man Utd – 13.18km

Christian Eriksen – TOTTENHAM vs Swansea – 13.17km

Harry Kane – TOTTENHAM vs Swansea – 13.12km

Marouane Fellaini – MAN UTD vs Southampton – 13.12km

No comments: