Baadhi ya wanaharakati wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi linaloshikiliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe, leo wamezungumza na wanahabari kuhusu kumnadi mgombea anayetaka kuwa mrithi wake jimboni kwake.
Akizungumza katibu wa wanaharakati hao, Daudi Bernard alisema kuwa kwa muda aliokaa madarakani Mhe Membe hakuna mabadiliko yoyote hivyo asiwapangie mtu wa kuwaongoza katika uchaguzi ujao.
‘’Tunamuomba Mhe Membe asitulazimishe kumchagua mtu anayemtaka yeye ambaye ni Katibu Mwenezi na Itikadi wa Taifa wa CCM, Nape Nnauye kama mrithi wake, kwa sababu hakuna huduma bora za jamii kama afya, barabara, shule ambazo zmetuletea,” alisema Bernard.
No comments:
Post a Comment