MBOWE KUTIKISA MWANZA KESHO - LEKULE

Breaking

28 Feb 2015

MBOWE KUTIKISA MWANZA KESHO

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema,  Alfred Rwakatare akitoa maelekezo



Walinzi wa Chadema wakiwa katika picha ya pamoja.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

MWENYEKITI  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe  anatarajia kufanya mkutano mkubwa hapa jijini Mwanza kesho kwenye Uwanja wa Furahisha lengo likiwa ni kuzungumza na wanachama wa chama hicho waliopo jijni hapa.
Akizungumza  mtandao wa  Global Publishers, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema,  Alfred Rwakatare  amesema kuwa mkutano huo utatikiza Mwanza kwa sababu utahudhuriwa na watu wengi na utakuwa  wa amani na wanatarajia kuzungumza na wafanyabiashara wadogowadogo ili kuwawezesha kufanya biashara zao bila kubughudhiwa na mtu.
“Licha ya Mheshimiwa Mbowe pia kutakuwepo na wabunge mbalimbali wa chama chetu  akiwemo mwenyeji wetu wa Jimbo la Nyamagana, Ezekia Wenje na  maandalizi makubwa yanaendelea kufanywa na chama chetu,” alisema Rwakatare.




No comments: