Manchester United yawika - LEKULE

Breaking

28 Feb 2015

Manchester United yawika




Mkwaju wa penalti uliofungwa na nahodha Wayne Rooney uliisaidia Manchester United kuichapa Sunderland mabao 2-0 baada ya West Brown kupewa kadi nyekundu katika kile kilichoonekana kama maonevu.

Rooney alifunga baada ya mshambuliaji Radamel Falcao kuchezewa visivyo na kusababisha kutolewa kwa Wes Brown badala ya John Oshea aliyecheza vibaya licha ya pingamizi kutoka kwa mashabiki.

Manchester united iliongeza bao la pili baada ya Rooney kufunga kupitia kichwa baada ya mkwaju wa Adnan Januzaj kupanguliwa na kipa.

Ushindi huo umeimarisha harakati za kilabu hiyo kuwania nafasi nne bora katika ligi hiyo.

Matokeo mengine:

West Ham 1 - 3 Crystal Palace

Burnley 0 - 1 swansea

Newcastle 1 - 0 Aston Villa

Stoke 1 - 0 Hull

West Brom 1 - 0 Southampton

No comments: