Arsenal ilinusurika dakika za lala salama na kuweza kuishinda Crystal Palace mabao 2-1 kabla ya kupanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza.
Carzola aliiweka Arsenal kifua alipofunga mkwaju wa penalti baada ya Pape Soure kumuangusha Danny Welbeck.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza alihusika katika bao la pili la kilabu yake baada ya mkwaju wake kupanguliwa naye Giroud kufunga bao la pili.
Wakati huohuo mchezaji wa Chelsea Nemanja Matic alipewa kadi nyekundu,huku viongozi hao wa ligi wakitoka sare ya 1-1 dhidi ya Burnley.
Branislav Ivanovic aliiweka Chelsea kifua mbele baada ya kufunga krosi ya Eden Hazard.
Burnley walisawazisha kupitia kona iliopigwa katika dakika za lala salama.
Na hayo yakijiri kilabu ya Manchester United ilipata pigo baada ya Swansea kufunga bao la dakika za mwisho kupitia mchezaji Bafetimbi na kuibuka kidedea kwa mabao 2-1.
Andre Herrera alikuwa ameiweka mbele Manchester United ,lakini wenyeji walijibu kupitia mchezaji Ki Sung Yeung aliyepata krosi ya Jonjo Shelvey.
Kikosi cha Louis Van Gaal kilitawala mchezo katika kipindi cha pili lakini kikashindwa kuona lango la Swansea.
Matokeo mengine ni haya yafuatayo:
Aston Villa 1 - 2 Stoke
Hull City 2 - 1 QPR
Sunderland 0 - 0 West Bromwich
No comments:
Post a Comment