Langa langa yazindua magari mapya - LEKULE

Breaking

3 Feb 2015

Langa langa yazindua magari mapya


Michuano ya magari ya Fomula one maarufu kama Langa Langa imezindua magari mapya ya mchezo huo na tayari yamesha anza kufanyiwa majaribio na timu tatu ziliingia barabarani katika mechi ya majaribio ya magari hayo.

Makampuni makubwa ya utengenezaji magari hayo ambao ni mabingwa kwa kazi hiyo duniani ni Mercedes, Red Bull Williams walianika wazi ubunifu mpya wa magari hayo katika mpango kazi wa kuanza kuyatumia magari hayo.

Magari hayo mapya yametengenezwa na vikosi nane kwa kutumia muda wa mwezi mmoja mjini Jerez ,na majaribio hayo yanalenga kuangalia kama mwezi huo mmoja wa ubunifu umefaulu ama lah.

Kampuni ya Force India wao wameshindwa kuonesha ubunifu wao mpya kwa mwaka huu imechelewa kutoka.

Makampuni haya ya Red Bull, Mercedesna Williams wao tayari hata picha za magariu hayo mapya zimekwisha tolewa .

Kipya utakachoshuhudia katika ubunifu huu mpya ni muundo wa pua ya magari hayo,pampa zimefanya mabadiliko ya mtazamo wa mbele wa magari hayo lakini zaidi ya hayo kipya utakacho shuhudia pindi ukiyaona magari hayo ni muonekano wa gari yenyewe anasema haya mkuu wa matengenezo wa magari ya Red Bull Rob Marshall,anasema kuwa kazi kubwa iliyofanywa huwezi kuiona kwa macho kirahisi, lakini kazi kubwa imefanywa juu ya magari hayo.

Kulinganisha na mwaka uliopita ,kampuni la magari la Mercedes wao gari yao inaonesha utofauti wa wazi kabisa ikijumuisha pua nyembamba na ndefu na body ya kipekee kabisa ya ubunifu wao.

Kubwa kuliko yote makampuni haya ya magari ya mashindano walinuia kutengeneza magari ambayo yana kasi zaidi,yenye ufanisi zaidi,yanayoaminika mchezoni na kikubwa kuliko yote ni magari yaliyo salama zaidi.

No comments: