Ligi ya mabigwa wa ulaya itaendelea tena leo kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja vya St. Jakob-Park na Veltins Arena.
Real Madrid watakua ugenini nchi Ujerumani kuwakabilia Schalke 04 katika mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Veltins Arena,
ambako Msimu uliopita kwenye hatua kama hii ya Mashindano haya haya Real iliwachapa wa Schalke 6-1.
Schalke wako chini ya Meneja Roberto Di Matteo huenda ikawosa Nyota wake Julian Draxler, Leon Goretzka na Jefferson Farfan walio majeruhi.
Huku Real Madrid ikiwakosa wachezaji wake mahiri , James Rodriguez na Luca Modric na Beki Sergio Ramos.
Mchezo mwingine utazikutanisha FC Basel dhidi ya FC Porto mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Jakob –Park
Ambapo Fc basel watakua nyumbani kuwaalika Wareno wa Fc Porto amabo hawakupoteza mchezo hata mmoja katika hatua za awali.
No comments:
Post a Comment