Kesi
ya kumdhuru mfanyakazi wa ndani inayomkabili raia wa Ufaransa,
Folkertsma Laurent (41), imeahirishwa hadi Machi 31, mwaka huu kutokana
na shahidi kutofika mahakamani.
Awali,
Wakili wa Serikali, Felista Mosha wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala,
alidai kwamba kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba
shahidi waliyemtegemea mahakamani hapo hakufika.
Pia
alidai kuwa shahidi huyo alipewa onyo afike mahakamani hapo ili
kuendelea na ushahidi huo lakini hakufanya hivyo na kwamba hakutoa
taarifa.
Hakimu
Mkazi Mwandamizi, Juma Hassani aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 31,
mwaka huu upande wa Jamhuri utakapoendelea kusikiliza kesi hiyo.
Hata
hivyo, mshitakiwa huyo alidai kuwa Wakili anayemuwakilisha alipatwa na
msiba hivyo alisafiri lakini mpaka anafika mahakamani hakujua kama
amesharudi au la.
Ilidaiwa
Mei 23, mwaka huu, maeneo ya Tabata Liwiti Wilaya ya Ilala, Laurent
alimpiga na kumsukuma Aneth Mponzi na kumsababishia maumivu mwilini.
Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment